EECC center Co-creation workshop at Vwawa District hospital

Siku ya Ijumaa, tarehe 27 Juni 2025, timu kutoka EECCiT MUHAS ilisafiri hadi mkoani Songwe kwa ajili ya warsha maalumu ya kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji na timu ya wafanyakazi wote wa Hospitali ya Wilaya ya Vwawa, ambayo imechaguliwa kuwa kituo kikuu cha utekelezaji wa utoaji wa tiba okovu na huduma msingi kwa wagonjwa mahututi (Essential Emergency and Critical Care, EECC).

Lengo la warsha hii lilikuwa kujadili kwa pamoja namna bora ya kufanikisha dhamira ya kuhakikisha kila mfanyakazi anaelewa na kutekeleza dhana hii adhimu ya EECC ambayo kimsingi ni utaratibu rahisi, nafuu na unaookoa maisha.

Pia, warsha hii ililenga kuifanya Hospitali ya Wilaya ya Vwawa kuwa mfano bora wa utekelezaji utaratibu huu wa EECC hapa Tanzania

#poetictanzania #eeccglobal #uniceftz #criticalcare #savinglife

Share the Post: