Published in Mwananchi Newspaper — Tanzania has cut in-hospital mortality by 31% through its Essential Emergency and Critical Care (EECC) program

Imechapishwa katika Gazeti la Mwananchi✍️

Tanzania imepunguza vifo vya wagonjwa waliolazwa hospitalini kwa asilimia 31 kupitia mpango wa Tiba Okovu na Huduma Msingi kwa Wagonjwa Mahututi (EECC), unaotekelezwa katika vituo 79 vya afya katika mikoa mitano ya Tanzania Bara na Zanzibar. Vifo vilipungua kutoka 116 hadi 81 kwa kila wagonjwa 10,000, utoaji wa huduma muhimu uliongezeka kutoka asilimia 27 hadi 75, na uelewa wa watumishi wa afya uliongezeka karibu mara mbili, baada ya mafunzo kwa zaidi ya watumishi 1,000. Ukiongozwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na MUHAS, UNICEF, na Global Affairs Canada, EECC unathibitisha kuwa kuimarisha huduma za msingi ikiwemo kutambua mapema, matibabu ya wakati, na vifaa muhimu , kunaweza kuokoa maisha ya maelfu, hata bila kupanua uwezo wa ICU.

——

Published in Mwananchi Newspaper — Tanzania has cut in-hospital mortality by 31% through its Essential Emergency and Critical Care (EECC) program, now running in 79 health facilities across five regions in Tanzania Mainland and Zanzibar . Deaths fell from 116 to 81 per 10,000 admissions, essential care delivery rose from 27% to 75%, and healthcare worker knowledge nearly doubled, after training over 1,000 frontline workers. Led by the Government of Tanzania with MUHAS, UNICEF, and Global Affairs Canada, EECC proves that strengthening basic critical care through early recognition, timely treatment, and essential equipment can potentially saves thousands of lives even without expanding ICU capacity.

Share the Post: