Pongezi Hospitali ya Wilaya ya VWAWA, EECC Center ya kwanza, Tanzania.ππΌππ½
Katika warsha ya EECC hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Hospitali ya wilaya ya Vwawa mkoani Songwe, ilitunukiwa nishani ya pongezi kwa kuboresha huduma za EECC kwa wagonjwa mahututi, kuongeza uwezo kwa watoa huduma na upatikanaji wa vifaa vya EECC.
Hospitali hii iliteuliwa kama kituo cha umahiri wa EECC, nakuwezeshwa kutoa EECC kwa 100%.
Pongezi nyingi kwa serikali kupitia Wizara ya Afya na TAMISEMI, Mganga mkuu wa mkoa wa songwe na team yake nzima kwa ushirikiano uliotukuka katika kuiwezesha Vwawa kuwa hospitali ya mfano kwa ubora wa EECC.
Tunawashukuru pia watoa huduma wote wa Vwawa na msimamizi wa EECC Dr. Uswege kwa kazi kubwa waliyofanya kufanikisha hili.